" Freely you have received, freely give " (Matthew 10:8)

НАЧАЛНА СТРАНИЦА   |  КАРТА НА САЙТА  |  КОНТАКТИ C HAC  |  ПОМОЩ    
Проучване на Библията Безплатни християнски книги Безплатни християнски е-книги За нас
  БЕЗПЛАТНА e-книжна версия на Суахили език издание 15

 

Mfululizo wa Paul C. Jong Juu ya Ukuaji wa Kiroho Kitabu cha 4:
Waraka wa Kwanza wa Yohana (II)

 • Електронната книга на формата : MS Reader
 • Текущи Изтегляния : 0
 • За тази книга
 • Съдържание
 

Dokezo

Mfululizo wa Paul C. Jong Juu ya Ukuaji wa Kiroho Kitabu cha 4 : Waraka wa Kwanza wa Yohana (II)

Maelezo ya Kina

Kama wewe ni Mkristo wa kweli, basi unapaswa kuufahamu upendo wa Mungu kwa uhalisia kuliko kuufahamu kwa nadharia tu. Wale wanaomfahamu na kumwamini Yesu kuwa ni Mwokozi wao ni lazima waufahamu upendo wa Mungu kwa uthabiti hasa kuhusiana na ondoleo la dhambi zao ambalo lilitimizwa kupitia Neno la injili ya maji na Roho. Ili tuweze kuufahamu upendo wa Mungu kwa kina basi tunapaswa kuwa waamini tunaoamini katika injili hii ya kweli. Upendo wa Mungu unajidhihirisha kwa kina na kwa uthabiti katika injili hii ya kweli. Kama tutaufahamu upendo wa Mungu, basi ufahamu wetuni lazima utokane na upendo thabiti wa Mungu kwetu sisi ambao umefunuliwa katika Ukweli wa injili ya maji na Roho. Ni hapo ndipo tunapoweza kuwaongoza wengine kuuendea upendo wa kweli wa Mungu.
Mtume Yohana anashuhudia kuwa Yesu Kristo, aliyekuja kwa maji, kwa damu, na kwa Roho Mtakatifu, ni Mungu Mwokozi mwenyewe. Kiini cha ushuhuda wake ni ule Ukweli wa ondoleo la dhambi, ambao unapatikana katika maji, damu, na Roho Mtakatifu.
Kama ilivyoandikwa katika Neno la Mungu, maji yana maanisha ni ubatizo wa Yesu alioupokea toka kwa Yohana Mbatizaji, na damu ina maanisha ni hukumu ambayo Yesu aliipokea kwa ajili ya dhambi zetu zote. Pia, ushahidi wa wokovu wetu unajikita katika Roho Mtakatifu, maji, na damu (1 Yohana 5:8). Huduma za maji, damu, na Roho Mtakatifu ni za Mungu na ambazo kwa hizo amewakomboa wenye dhambi toka katika dhambi zao zote.

Kutoka kwa Mchapishaji

Suala la msingi ambalo tunapaswa kulitambua ni kuwa Yesu aliupokea ubatizo wa Yohana Mbatizaji katika Mto Yordani ili aweze kuzichukua dhambi za ulimwengu katika mwili wake kabla ya kusulubiwa Msalabani. Lakini pamoja na ukweli huo, kuna tatizo kubwa kwa kuwa watu wengi bado hawaufahamu ukweli huu. Hivyo, tunapaswa kuzingatia kuwa ubatizo wa Yesu ulikuwa na lengo la kuzichukua dhambi za ulimwengu katika mwili wake mara moja kabla ya kusulubiwa Msalabani. Hivyo kumfahamu na kumwamini Yesu Kristo kuwa ni Mwokozi wetu, aliyekuja hapa duniani kwa injili ya maji na Roho, ni muhimu sana kwa ajli ya kuzitoweshea mbali dhambi zetu.


 

 
Безплатни християнски е-книги
    Списък на е-книгите
    Суахили издание 15
 
 • За тази книга
 •  
 • Съдържание
 •     Какво e е-книга?
   
 • За е-книгата
 •  
 • Как да чета е-книга?
 •  
 • Често задавани въпроси
 •  
 • Помощ за изтегляне
 •     Четци за е-книги
   
 • MS Reader 2.0
 •  
 • Acrobat Reader 4.0
 •  

  Регистрирай се като сътрудник
  Зоната на съдружника
  Bookmark
     
  Copyright © 2001 - 2020 The New Life Mission. All Rights Reserved.